Product description
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo laSayansi na Teknolojia kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo la Sayansi na Teknolojia kwa Darasa la Saba wa mwaka 2019 uliotole
..
read more
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo laSayansi na Teknolojia kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo la Sayansi na Teknolojia kwa Darasa la Saba wa mwaka 2019 uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kitabu hiki kinalenga kuendelea kukuza na kujenga umahiri wa stadi za udadisi, ubunifu, uchunguzi na ugunduzi. Aidha, kitabu hiki kina sura 10 ambazo ni: Alama za usalama katika mazingira, Nishati ya umeme, Kuelea na kuzama kwa vitu, na Antena. Sura nyingine ni Mashine tata, Majaribio ya kisayansi, Kuteketeza taka, Afya ya mwili, Mfumo wa fahamu, na Mfumo wa upumuaji. MaiJdhui katika kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya maelezo, vielelezo, kazi za kufanya na majaribio. Kitabu kimesheheni mazoezi yaliyoandaliwa kwa lengo la kupima uelewa wa mwanafunzi katika kila sura. Unapaswa kufanya kazi zote zilizomo katika kitabu hiki pamoja na kazi nyingine utakazopewa na mwalimu, ili uweze kukuza umahiri uliokusudiwa.
read less