Product description
Ni mpaka pale ndoto yao hii ya utajiri wa haraka inapbwageukia na kuwa jinamizi la kutisha, ndipo wanapobaini kuwa walikuwa wamecheza patapotea kwa kukichokoza kifo chenye uchu. Kinachofuatia ni saa 72 za kufa ama kupona, wanajikuta wakihaha huku na
..
read more
Ni mpaka pale ndoto yao hii ya utajiri wa haraka inapbwageukia na kuwa jinamizi la kutisha, ndipo wanapobaini kuwa walikuwa wamecheza patapotea kwa kukichokoza kifo chenye uchu. Kinachofuatia ni saa 72 za kufa ama kupona, wanajikuta wakihaha huku na huko, usiku na mchana, mjini na msituni, katika mchakamchaka wa kunusuru uhai wao.
Anapotokea Mzee Shata na ahadi ya kuwanusuru kwenye kifo kinachowakabili, wanajikuta butwaani pale wanapogundua kuwa yawapasa kwanza kukikabili kisanga kingine ndio wanusurike, ilhali muda ukizidi kuwatupa mkono.
Wanapokutana na mtu mwingine aitwaye Tarik Dizzo ndipo mchakamchaka wao uliowagharimu machozi, jasho na damu unapoingia kwenye mtanziko mkubwa unaomlazimu Morena kuamua kati ya utajiri, uhai, na mapenzi ... kipi kina thamani zaidi?
KIROBA CHEUSI ni simulizi isiyopaswa kukoswa, ikiwa imesheheni visa vya kusisimua, mikasa ya kuogofya, taharuki za kushtukiza na mipasho ya kufurahisha huku ikijikita kwenye thamani ya urafiki wa kweli.
read less