Tab Article
Kitabu hiki ni cha nne katika mfululizo wa vitabu vya somo la Sayansi na Teknolojia. Kitabu hiki kimeandaliwa mahususi kwa ajili ya mwanafunzi wa Darasa la Sita. Kitabu kinalenga kuendelea kukuza na kujenga umahiri wa stadi za uchunguzi, ugunduzi, udadisi na ubunifu.
Kitabu hiki kina sura kumi na nane zilizoandaliwa kukidhi mahitaji ya muhtasari wa somo la Sayansi na Teknolojia kwa Darasa la Sita. Sura hizo ni: Hewa, Ukuaji wa mimea, Usanishaji chakula, Udongo, Nishati ya umeme, Nishati jadidifu, Mashine na kazi, Uyeyushaji mweneo na Programu jedwali. Sura nyingine ni: Intaneti, Usafi na mazingira, Huduma ya kwanza, Magonjwa ya ngono, virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Magonjwa ya kurithi, Huduma ya afya, Mfumo wa mzunguko wa damu,Balehe na Mfumo wa uzazi.
Maudhui katika kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya maelezo, vielelezo, kazi za kufanya na majaribio. Kitabu kimesheheni mazoezi yaliyoandaliwa kwa lengo la kupima uelewa wa mwanafunzi katika kila sura. Vilevile, kitabu kimelenga kumwongezea mwanafunzi uwezo wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.