Tab Article
Kitabu hiki ni cha pili katika mfululizo wa vitabu vya Stadi za Kazi ambacho kimeandaliwa mahususi kwa mwanafunzi wa Darasa la Sita. Kitabu hiki kimelenga kukuza umahiri wa stadi za uchunguzi, ugunduzi, udadisi, ubunifu, kusoma, kuandika na kuhesabu. Aidha, kitabu hiki kina sura tisa zilizoandaliwa kukidhi mahitaji ya muhtasari wa somo linalohusika. Sura hizo ni: Unadhifu; Utunzaji wa mazingira; Upishi; Ala za muziki; Kumudu misingi ya uigizaji; Picha, vichezeo na uchapaji; Ufinyanzi, ususi na vifani; Stadi za ujasiriamali; na Usimamizi wa fedha. Kitabuhiki kinawasilisha maudhui kwa njia ya habari, picha, kazi za vitendo na mazoezi.