Tab Article
Fungate ya Uhuru ni diwani ya mashairi yanayofichua madhila wafanyiwayo
wanyonge na baadhi ya wakubwa, hasa viongozi wanyonyao jasho la wananchi na
kujineemesha migongoni mwa wakulima na wafanyakazi. Mashairi haya yanaonesha
hasira aliyonayo mwandishi kwani “wakubwa†hawa wanaendelea kujistarehesha
huku wakulima na wafanyakazi, ambao ndiyo wajenga nchi, wakiendelea kudidimia
katika lindi la dhiki. Hakika, mashairi haya yatamfanya msomaji atafakari uelekeo wa
nchi yetu na hapohapo kumchokoza atafute ufumbuzi wa “uyabisi†huu!
Kitabu hiki ni tunu kwa wote wapendao ushairi bora na wenyekupenda kutathmini
mwelekeo wa jamii zetu. Vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili shuleni na vyuoni
watanufaika na sanaa ya mwandishi katika ushairi huu wenye vionjo maridhawa.
Dr. Muhammed Seif Khatib alizaliwa mwaka 1951, Umbuji, ZanzÃbar. Alisomea
Ualimu katika Chuo cha Nkrumah, ZanzÃbar. Mnamo mwaka 1978 alihitimu
shahada ya B.A. (Ed.) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kisha alitunukiwa shahada ya
uzamili (M.A.) katika Chuo Kikuu cha London (S. O.A .S ) mnamo mwaka 1982.
Mwaka 2011 alifaulu shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Aidha yeye ni mwandishi maarufu wa makala na mtunzi wa vitabu kadhaa vya ushairi
wa Kiswahili kama vile: Ukombozi wa ZanzÃbar (OUP 1975 ); Pambazuko la Afrika
(E.A.P 1982), Taarabu ZanzÃbar (T.P.H. 1992), Wasakatonge (OUP, 2003), Chanjo
( TUKI, 2014) na Vifaru Weusi (Vide-Muwa, 2016).
Khatib ameshawahi kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Muungano katika awamu tofauti katika
Serekali ya Jamuhri ya Muungano. Kwa sasa Dkt.Muhammed Seif Khatib ni
mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.