Categories: Plays, short stories and poetry

Hidaya ya Shaaban Robert 5

18,000 TZS

Product description

PAMBO LA LUGHA
Huu ni mkusanyiko wa mashairi ya Shaaban Robert unaoakisi maisha ya jamii kwa kuangazia nyanja mbalimbali na mabadiliko yake. Diwani hii pendwa imedhihirisha umaarufu na utamu wake kwa kutajwa na kunukuliwa katika majukwaa mbalimbali

Qty

Tab Article

PAMBO LA LUGHA
Huu ni mkusanyiko wa mashairi ya Shaaban Robert unaoakisi maisha ya jamii kwa kuangazia nyanja mbalimbali na mabadiliko yake. Diwani hii pendwa imedhihirisha umaarufu na utamu wake kwa kutajwa na kunukuliwa katika majukwaa mbalimbali ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Pambo la Lugha ni kitabu kilichopambwa si kwa dhamira na ujumbe tu, bali pia kwa mitindo inayovutia jicho la msomaji na kuibua tafakuri za msingi za maisha ya mwanadamu.

MASHAIRI YA SHAABAN ROBERT
Hii ni moja ya diwani fupi miongoni mwa kazi za Shaabab Robert inayozungumzia namna bora ya wanajamii kuwa na mahusiano bora na kujiletea maendeleo. Masuala mbalimbali kama vile dini, maadili na maisha kwa jumla yanazungumziwa humu na mwandishi. Chachu hii inaleta changamoto ya kujitahidi kupambana hadi ku kia malengo ya maisha bora ambayo ni ndoto ya kila mmoja. Hakika da na ya maisha iliyo chwa ina chuliwa katika diwani hii tayari kwa yeyote atakayeisoma.

TENZI ZA MARUDI MEMA NA OMAR KHAYYAM
Utungo huu umejaa tunu na mafunzo kwa jamii ukisawiri mwelekeo wa jamii kwa kutoa miongozo inayoweza kutumika kama reli za maisha ya kila siku. Marudi si marudi tu, bali yapaswa kuwa marudi mema yatakayokuwa msaada kwa jamii. Ungana na mtunzi ili kufaidi kazi hii yenye msisimko wa pekee unaoambatana na elimu mujarab kwa jamii.

0 reviews for Hidaya ya Shaaban Robert 5

Add a review

Your Rating