Product description
Kusudio la kitabu hiki ni kuweka kumbukumbu ya matukio mbalimbali ambayo, kwa pamoja, yanatengeneza Historia ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambao uliasisiwa mwezi Aprili, 1964.
Matukio muhimu yanayozungumziwa katika kitabu hiki, yameoneshwa k
..
read more
Kusudio la kitabu hiki ni kuweka kumbukumbu ya matukio mbalimbali ambayo, kwa pamoja, yanatengeneza Historia ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambao uliasisiwa mwezi Aprili, 1964.
Matukio muhimu yanayozungumziwa katika kitabu hiki, yameoneshwa katika orodha ya YALIYOMO Kuna aina tofauti za uandishi wa Historia. Kwa mfano, kuna aina ya uandishi wa Historia ambayo huishia katika kusimulia matukio husika. Tofauti na aina hiyo ya uandishi, kitabu hiki kimekwenda mbali zaidi ya kusimulia matukio yenyewe, kwa kueleza vilevile sababu halisi za matukio hayo. Kwa mfano, tumeeleza sababu za msingi zilizochochea kuwapo kwa Muungano huu; na sababu za usiri uliofunika mchakato huo hadi wakati wa kusaini Mkataba wa Makubaliano ya kuunda Muungano huu. Vilevile tumeeleza sababu za msingi zilizomfanya Mwalimu Nyerere, pamoja na chama Tawala, kuendelea kukataa majaribio yote ya kubadilisha muundo wa Muungano huu na kuufanya uwe wa serikali tatu badala ya mfumo wa Serikali mbili.
read less