Product description
A. Outline of the book
The book, written in Kiswahili, has the following 7 chapters:
1. Asili, umbile la mmea na mahitaji muhimu kwa kilimo cha Viazi Mviringo.
2. Umuhimu na matumizi ya Viazi Mviringo.
3. Uchaguzi wa mbegu bora na matayarisho yake kw
..
read more
A. Outline of the book
The book, written in Kiswahili, has the following 7 chapters:
1. Asili, umbile la mmea na mahitaji muhimu kwa kilimo cha Viazi Mviringo.
2. Umuhimu na matumizi ya Viazi Mviringo.
3. Uchaguzi wa mbegu bora na matayarisho yake kwa ajili ya kupanda.
4. Utayarishaji wa shamba, upandaji wa mbegu na udhibiti wa magugu.
5. Wadudu waharibifu na udhibiti wake, magonjwa na udhibiti wake.
6. Ukomaaji, uvunaji, uchambuzi, upangaji gredi, ufungaji, usafirishaji, uimarishaji ngozi na hifadhi.
7. Usindikaji wa Viazi Mviringo.
Brief Summary
This book is on How to Grow Round Potatoes.
B. Maelezo mafupi ya kitabu:
Katika kundi la mazao ya mizizi, Viazi Mviringo ni maarufu na vina umuhimu wa pekee. Ni zao la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Zao hili ni moja ya mazao manne ya chakula yanayozalishwa kwa wingi na kutumiwa na watu wengi duniani. Mbali na utamu wa Viazi Mviringo, lakini, mlaji hujipatia asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Aidha, vina kiasi cha kutosha cha protini, madini, vitamini na maji. Umaarufu wake unaongezeka kila kukicha. Watoto, vijana na watu wazima hupenda kula viazi mviringo kama chipsi, viazi vilivyopondwapondwa, viazi vilivyochemshwa n.k “Chipsi na kukuâ€, chipsi na mayaiâ€, “chipsi na nyama†au “chipsi kavu†ni majina maarufu sana katika familia nyingi, migahawa, hoteli, mama lishe n.k., hasahasa, kwa watoto, vijana na watu wasiokuwa na muda wa kusubiri vyakula vinavyochukua muda mrefu kuviandaa. Kwa sababu hii, mahitaji ya zao hili ni makubwa sana na bei yake huongezeka mara kwa mara. Lengo la kitabu hiki ni kuwawezesha wakulima wengi zaidi walistawishe kwa kufuata kanuni bora, wajue jinsi ya kulitayarisha na kulisindika.
read less