Product description
Huu ni mchezo wa saba katika mfululizo wa vitabu vya michezo ya kuigiza kutoka Tanzania Publishing House. Michezo hii imeendelea kuburudisha na kuelimisha wasomaji wa rika zote tangu ilipochapishwa kwa mara ya kwanza. Kitabu hiki kama vingine katika
..
read more
Huu ni mchezo wa saba katika mfululizo wa vitabu vya michezo ya kuigiza kutoka Tanzania Publishing House. Michezo hii imeendelea kuburudisha na kuelimisha wasomaji wa rika zote tangu ilipochapishwa kwa mara ya kwanza. Kitabu hiki kama vingine katika mfululizo huu kimechaguliwa kufundishia Lugha na drama mashuleni. Kijiji Chetu ni mchezo wa kuigiza juu ya kijji chenye uongozi mbaya. Kama inavyoeleweka ngao ya wakulima ni ushirika. Wakati ushirika huo haupo na maendeleo nayo hayapatikani au yatakuwa mashakani. Mchezo huu unamulika baadhi ya sababu za msingi zinazozuia kukua Kwa ushiriki zikiwemo ubinafsj, ulaghai, uzembe na ufisadi. Mwandishi wa mchezo huu Bwana Ngalimecha Ngahyoma ni mkurugenzi wa vipindi maalumu Shirika la Utangazaji Tanzania-TBC, na ni mwandishi wa mchezo mwingine, uliochapishwa na Tanzania Publishig House uitwao Huka.
read less