Product description
Kalabweli alitarajia kuwa angewatunza wazazi wake,dada na wadogo zake.Na kwa kweli kalabweli alifanikiwa katika biashara,akashamiri,akapenda na kupendwa,akaijua pesa………..
Kisiki kikavu kinatufunulia maisha ya Kalabweli ambayo yamebe
..
read more
Kalabweli alitarajia kuwa angewatunza wazazi wake,dada na wadogo zake.Na kwa kweli kalabweli alifanikiwa katika biashara,akashamiri,akapenda na kupendwa,akaijua pesa………..
Kisiki kikavu kinatufunulia maisha ya Kalabweli ambayo yamebeba historia ya UKIMWI huko mkoani Kagera.Historia iliyoanzia katika umasikini uliofuatia vita vya Iddi Amin,hali iliyozaa biashara ya magendo na maisha ya starehe iliyokithiri.UKIMWI ukabisha hodi ukapatiwa majina;Juliana,Silimu;Ninja…………
Kisiki Kikavu kinaweka wazi udhaifu wetu katika kukabili changamoto za maisha.Jinsi unavyozidi kusoma kisiki Kikavu ndivyo unavyoona kwamba historia,siasa,mila na uchumi vimeshikamana katika kuibua na kutandawaza janga la UKIMWI,na hapo unagundua ukavu wa fikra za mwanadamu.
Hii ni riwaya ya aina yake inayochambua taathira za vvu,uelewa wa watu,ukubalifu wao na jinsi tabia zinavyobadilika kwa wakati ,na kwa rika .Ni riwaya ninayopendekeza isomwe na kila mmoja anayetaka kujua undani changamoto inayotukabili kuhusu UKIMWI
read less