Tab Article
Kitabu hiki kinafundisha somo la Kiswahili kulingana na Muhtasari mpya wa Elimu ya Msingi kwa Darasa la 4 wa mwaka 2020. Uandaaji wa kitabu hiki umezingatia misingi na vigezo vya uandishi bora na umelenga kumhamasisha mwanafunzi kupenda kujifunza zaidi. Kitabu hiki kina hadithi, midahalo, risala na mazoezi mengi ambavyo kwa pamoja vinampa mwanafunzi fursa ya kujifunza na kujenga umahiri katika lugha ya kiswahili. Vipengele vinavyofundishwa katika kitabu hiki ni pamoja na Kusoma, Kuandika, Sarufi, Misamiati, Matumizi ya Kamusi, Hadithi fupi, Vitendawili, Nahau na Methali. Tuna imani kuwa kitabu hiki kitamjengea mwanafunzi uwezo na kumpa uwanja sahihi wa kujifunza somo la Kiswahili kwa vitendo.