Product description
Kitabu hiki kinafundisha somo la Kiswahili kulingana na Muhtasari mpya wa Elimu ya Msingi kwa Darasa la 5 wa mwaka 2020. Uandaaji wa kitabu hiki umezingatia misingi na vigezo vya uandishi bora na umelenga kumhamasisha mwanafunzi kufurahia somo la Kis
..
read more
Kitabu hiki kinafundisha somo la Kiswahili kulingana na Muhtasari mpya wa Elimu ya Msingi kwa Darasa la 5 wa mwaka 2020. Uandaaji wa kitabu hiki umezingatia misingi na vigezo vya uandishi bora na umelenga kumhamasisha mwanafunzi kufurahia somo la Kiswahili na kupenda kujifunza zaidi.
Kitabu hiki kina hadithi, mashairi, ngonjera, tenzi, insha na habari fupi lukuki zitakazompa mwanafunzi mazoezi ya kusoma, kuandika, misamiati na kufupisha kazi za aina hii. Vilevile, kitabu kina vitendo na mazoezi mengi ambavyo kwa pamoja vitamjengea mwanafunzi umahiri katika somo la Kiswahili. Vipengele vinavyofundishwa katika kitabu hiki ni pamoja na Mazungumzo, Kuwasilisha Taarifa, Uandishi wa Insha, Habari Fupi na Hadithi, Uandishi wa Barua, Ushairi, Tenzi na Ngonjera, Nyakati, Methali, Vitendawili na Nahau, Misamiati pamoja na Ufahamu na Ufupisho. Tuna imani kuwa kitabu hiki kitamjengea mwanafunzi uwezo na kumpa uwanja sahihi wa kujifunza somo la Kiswahili kwa vitendo.
read less