Product description
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Maarifa ya Jamii, kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba. Kitabu hiki, kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa Maarifa ya J
..
read more
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Maarifa ya Jamii, kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba. Kitabu hiki, kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa Maarifa ya Jamii wa mwaka 2019, uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kitabu hiki kimeandaliwa ili kukuwezesha kujifunza Majanga ya asili, Maendeleo ya binadamu na zana za uzallshaj mali, Tabianchi ya Tanzania, Mila na desturi za Watanzania, Usafirishaji na uhusiano wa Tanzania na nchi nyingine, Athari za njia zilizotumika kudai uhuru Afrika, Maendeleo nchini Tanzania baada ya uhuru, Matumizi ya ramani, Mfumo wa Jua, Idadi ya watu na makazi, Shughuli za kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Ujasiriamali. Maudhui ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya matini, kazi za kufanya, ramani na picha zenye mvuto ambazo zote zinachochea ujenzi wa umahiri unaokusudiwa kwa kila sura. Vilevile, katika kila sura yapo mazoezi yenye lengo la kupima uelewa wako. Hivyo basi, unapaswa kufanya kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi zingine utakazopewa na mwalimu.
read less