Product description
Michezo na sanaa hupendwa sana na wanafunzi. Michezo na sanaa hufurahisha na kuelimisha. Vilevile, husaidia katika kufundisha masomo mengine. Katika Kusoma, Kuandika na Kuhesabu utatumia sanaa kwa namna mbalimbali.
Michezo iliyomo kitabuni ni michez
..
read more
Michezo na sanaa hupendwa sana na wanafunzi. Michezo na sanaa hufurahisha na kuelimisha. Vilevile, husaidia katika kufundisha masomo mengine. Katika Kusoma, Kuandika na Kuhesabu utatumia sanaa kwa namna mbalimbali.
Michezo iliyomo kitabuni ni michezo sahili, michezo ya jadi na viungo. Ipo pia michezo ya riadha na ya mipira. Michezo hii ni ile inayochezwa na watoto kila siku mitaani. Michezo na sanaa hizo zitarahisisha kuelewa vizuri Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Sanaa zilizopo ndani ya kitabu hiki zinahusu kuchora, kuumba herufi, kuumba tarakimu na kuzipamba. Vilevile, sanaa hizi zinahusu kupiga chapa, kuimba, kusimulia hadithi na kuigiza.
Soma kwa makini habari zilizorno kitabuni na uzielewe. Soma maswali na mazoezi uliyopewa. Jibu maswali na kufanya mazoezi hayo. Unaweza kupata msaada kwa watu mbalimbali. Kama wenzako, wazazi au walezi na walimu wako.
read less