Product description
Bila kujali umri, cheo ulichonacho, hadhi uliyonayo, sehemu unayoishi, rangi, taifa wala kabila, msongo wa mawazo humkuta kila mtu. Msongo wa mawazo upo kila mahali si kwa wanawake si kwa wanaume, si kwa watoto si kwa watu wazima, si kwa walio kwenye
..
read more
Bila kujali umri, cheo ulichonacho, hadhi uliyonayo, sehemu unayoishi, rangi, taifa wala kabila, msongo wa mawazo humkuta kila mtu. Msongo wa mawazo upo kila mahali si kwa wanawake si kwa wanaume, si kwa watoto si kwa watu wazima, si kwa walio kwenye ndoa, si kwa ambao hawajaingia kwenye ndoa. Walio kwenye ndoa wanakutana na msongo wa mawazo unatokana na changamoto za kawaida katika ndoa, kama vile kubalance/kusawazisha mahitaji ya ndoa na biashara/kazi, wengine hukabili changamoto ya malezi katika karne hii ya 21 inawafanya wawe na msongo wa mawazo. Walio single nao wana msongo wa mawazo, kwani wanajiuliza maswali mengi na mengine yasio na majibu, mfano, nitaolewa na nani? Je, huyu niliye naye kwenye mahusiano ni mtu sahihi? Na vipi ikitokea tumeachana na wakati nimekaa naye zaidi ya miaka minne? Hivi huko kwenye ndoa kukoje natamani niolewe/nioe na mimi nijonee mwenyewe. Baadhi ya marafiki zangu wengi wameshaoa au kuolewa bado mimi tu. Maswali kama haya na mengine mengi huleta msongo wa mawazo kwa watu ambao hawajaingia katika ndoa.
read less