Tab Article
Umahiri katika Historia ya Tanzania na Maadili ni kitabu kilichoandaliwa kwa kuzingatia maudhui ya Muhtasari wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili kwa Kidato cha Kwanza, mwaka 2023. Uwasilishaji wa mada na dhana mbalimbali katika kitabu hiki umezingatia ujenzi wa umahiri kama inavyopendekezwa katika mtaala mpya wa elimu wa Taifa. Kitabu kimehusisha vipengele vifuatavyo vinavyokifanya kiwe chaguo sahihi kwa kila mwanafunzi na mwalimu wa somo la Historia ya Tanzania na maadili:
• Bunguabongo kumsaidia mwanafunzi kutafakari kuhusu dhana mbalimbali za kihistoria.
• Kazi za kufanya ili kumpa mwanafunzi nafasi ya kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa kujifunza Historia na maadili ya Taifa lake.
• Vielelezo vya utosha kumsaidia mwanafunzi kuelewa kwa haraka zaidi dhana zinazoelezewa katika kitabu.
• Visamafunzo kwa ajili ya kumpatia mwanafunzi mifano halisi ya dhana zinazofundishwa na kujifunzwa darasani.
• Mazoezi ya marudio kila baada ya sura kumsaidia mwanafuzi kujipima kama ameweza kupata umahiri uliokusudiwa katika sura husika.
• Majaribio mwishoni mwa kitabu ili kumjengea mwanafunzi uzoefu wa kutosha kuhusu mitihani ya mwisho wa mwaka ya kitaifa.