Product description
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Uraia na Maadili kuanzia Oarasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Oarasa la Saba. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na Muhtasari wa Somo la Uraia
..
read more
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Uraia na Maadili kuanzia Oarasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Oarasa la Saba. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na Muhtasari wa Somo la Uraia na Maadili wa mwaka 2019 uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kitabu hiki kimezingatia mwenendo na matarajio ya nchi yetu ya Tanzania katika kukujengea wewe mwanafunzi uwezo wa kuheshimu na kuithamini jamii yako, kuwa mwajibikaji na mstahimilivu. Maudhui yaliyomo katika kitabu hiki ni mwendelezo wa yale yaliyomo katika kitabu cha Uraia na Maadili Darasa la Sita. Inatarajiwa kuwa, maudhui haya yatakujengea uwezo wa kuwa na tabia ya uadilifu, kupenda, na kudumisha amani katika nchi na kuweza kuishi vizuri na watu wa asili tofauti katika jamii. Kitabu hiki kina sura kumi na nne na kila sura imeundwa na vipengele kadhaa. Aidha, maudhui ya sura za kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya habari na vielelezo au picha. Kila sura ina mazoezi na kazi za kufanya zinazozingatia kujenga nyanja za maarifa (utambuzi), vitendo (stadi) na mwelekeo (maono). Hivyo basi unapaswa kufanya kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi zingine utakazopewa na mwalimu.
read less