Product description
Hidaya ya Penina Muhando ni mkusanyiko wa kazi mujarabu za mwandishi hodari wa tamthiliya, Profesa Penina Oniviel Muhando (Pia, Penina Mlama), ambaye, kwa mchango wake adhimu katika lugha ya Kiswahili, hususan utanzu wa tamthiliya, anastahili kutambu
..
read more
Hidaya ya Penina Muhando ni mkusanyiko wa kazi mujarabu za mwandishi hodari wa tamthiliya, Profesa Penina Oniviel Muhando (Pia, Penina Mlama), ambaye, kwa mchango wake adhimu katika lugha ya Kiswahili, hususan utanzu wa tamthiliya, anastahili kutambuliwa kama Mama wa Tamthiliya ya Kiswahili. Mbali ya kuwa tunu zenye kubeba masimulizi ya historia, kra, desturi na mapito ya jamii, kazi hizi zimetoa mchango mkubwa katika kukuza matumizi na umaarufu wa lugha ya Kiswahili duniani.
Mkusanyiko huu unalenga kuhakikisha kuwa kazi hizi adhimu za Kiswahili zinahifadhiwa na kuenezwa kote ulimwenguni kama shajara ya fasihi, historia, maarifa na harakati za Mwafrika. Sambamba na dhamira hii, mkusanyiko huu na mingine ya aina hii inatoa haki stahiki ya kuwaenzi kikamilifu watunzi wetu mashuhuri kwa mchango wao mkubwa katika lugha na fasihi ya Mwafrika.
Hidaya ya Penina Muhando ina jumla ya juzuu mbili (2) ambazo, kwa pamoja, zimebeba kazi 9 za mwandishi huyu mbuji wa Tamthiliya na mwanaharakati nguli wa sanaa ya Mwafrika, lugha ya Kiswahili, na usawa wa kijamii, Profesa Penina Oniviel Muhando.
Nguli huyu wa Kiswahili anatambuliwa kuwa mwandishi wa kike wa Tamthiliya za Kiswahili mwenye machapisho mengi zaidi na ambaye ametoa mchango mkubwa katika kujenga msingi wa elimu ya uandaaji wa Tamthiliya na kukuza ustawi wa sanaa za maonyesho za Mwafrika. Kama mtunzi hodari, mwalimu mahiri na msanii mwenye kipaji cha kipekee, Penina Muhando anajivunia wabobevu wengi kabisa wa Kiswahili, hasa katika utanzu wa Tamthiliya, ambao wamepita katika mikono yake na kunyangwa kuwa wanafasihi thabiti na watetezi wa lugha na utamaduni wa Mwafrika
read less