Product description
ASHIKI KITABU HIKI
Hii ni diwani yenye mashairi mbalimbali yanayojadili mambo tofauti ya maisha ya binadamu. Kwa jumla kitabu hiki kinampa msomaji elimu muhimu ya namna ya kupambana na maisha yake katika hali zote, njema na mbaya. Msomaji anaaswa ku
..
read more
ASHIKI KITABU HIKI
Hii ni diwani yenye mashairi mbalimbali yanayojadili mambo tofauti ya maisha ya binadamu. Kwa jumla kitabu hiki kinampa msomaji elimu muhimu ya namna ya kupambana na maisha yake katika hali zote, njema na mbaya. Msomaji anaaswa kutahadhari kwani maisha ni njiapanda ya wema na ubaya.
MAPENZI BORA
Kitabu hiki kinazungumzia mapenzi kama suala mtambuka. Mwandishi anaonesha ni namna gani mapenzi yanaweza kuwa na matokeo hasi au chanya kulingana na aina ya mapenzi yenyewe. Mwandishi anazungumzia hili kinaganaga kwa wasomaji wake akiwaasa kuwa macho na mapenzi pasi na ku sha umuhimu wake katika jamii.
INSHA NA MASHAIRI
Maisha ya binadamu yamejaa changamoto nyingi. Binadamu hana budi kupambana na kutatua changamoto hizo. Katika kitabu hiki mwandishi anatoa mifano mbalimbali ya changamoto na jinsi ya kupambana nazo. Kitabu hiki kimejaa maadili mbalimbali ambayo binadamu akiyazingatia ataishi maisha yenye furaha na amani tele.
read less