Categories: Plays, short stories and poetry

Joka la Mdimu

  • ISBN: 9789987701698
  • Publisher: APE Network
  • Availability: Out of stock
6,000 TZS

Product description

Tino alistakimu Kiungani Sega, nje kidogo ya jiji la Mindule. Alibangaiza kwa kuvuta kwama. Alikuwa na mke na watoto watatu. Mtoto wake mkubwa, Cheche (mvulana wa miaka 12) ghafla alivunjika kiuno katika michezo maalumu ya kusherehekea uhuru wa nchi

Qty

Tab Article

Tino alistakimu Kiungani Sega, nje kidogo ya jiji la Mindule. Alibangaiza kwa kuvuta kwama. Alikuwa na mke na watoto watatu. Mtoto wake mkubwa, Cheche (mvulana wa miaka 12) ghafla alivunjika kiuno katika michezo maalumu ya kusherehekea uhuru wa nchi yao. Baada ya kusota katika hospitali ya wilaya hali yake ilizidi kuzorota. Iliendelea hivyo hata pale alipoonana na Dakta Mikwala, bingwa wa mifupa katika hospitali kuu ya taifa jijini Mindule.
Kutokana na juhudi za Amani, sahibu yake Tino ambaye alikuwa dereva wa teksi jijini Mindule, Dakta Mikwala alipendekeza Cheche akatibiwe upesi katika hospitali mahsusi ya mifupa ya Glasgow, Uingereza ama sivyo Cheche angekuwa kiwete maisha yake yote. Sakata likawa kupata kibali cha kununua pesa za kigeni za matibabu na safari. Yote tisa, kumi ilibaki namna ya kuzipata pesa zenyewe!
Hadithi hii ni kielezeo cha matatizo makubwa ya kisiasa na uchumi yanayozikumba nchi nyingi zinazoendelea hususan Afrika. Inafaa sana kusomwa na wapenzi wa fasihi wa aina na daraja zote.

0 reviews for Joka la Mdimu

Add a review

Your Rating