Tab Article
Msingi na dafina ya tamthilia hii ni historia na lengo kuu la Mwalimu Julius Nyerere na TANU kutaka kujenga uchumi wa Ujamaa na Kujitegemea mintarafu mwongozo wa kitabu cha Azimio la Arusha, 1987. Tamthilia hii, pamoja na masuala mengine, inaangazia zaidi kuanzishwa kwa Vijiji vya Ujamaa nchini Tanzania na changamoto na matatizo yaliyojitokeza katika kuanzishwa kwake.
➢ Kwamba: Hata kama kinadharia, Azimio la Arusha lilionesha nuru na matumaini, lakini utekelezaji wake aghalabu, ulifanywa kwa kasi iliyowaelemea wanaume, wanawake na watoto.
➢ Kwamba: Wananchi wengi hawakupenda kuondoka katika vijiji vyao vya jadi.
➢ Kwamba: Vijiji vingi vipya havikuwa vijiji bali mapori yaliyokosa huduma muhimu kama hospitali, maduka, shule, barabara, n.k.
➢ Kwamba: Viongozi katika kutumia nguvu ya kupindukia, walijenga chuki na uhasama na wananchi. Mwandishi, katika tamthilia hii, anaonesha kwa kupitia visa halisi, mathalan, jinsi mkulima wa Isimani Wilayani Iringa, Mzee Mwamwindi, ambaye, baada ya kuzongwa kupindukia na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Wilbert Kleruu, siku ya tarehe 25/12/1971, alichukua bunduki yake akafyatua na kumuuwa Dkt. Kleruu. Hiki ni moja kati ya visa vingi vya ukweli ambavyo tamthilia hii imeviangazia kwa undan