Product description
Kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo wa vitabu vya Uraia na Maadili kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa darasa la tano. Kitabu kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa Uraia na Maadili wa mwaka 2016.
Kitabu kimezingatia mwenendo na matara
..
read more
Kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo wa vitabu vya Uraia na Maadili kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa darasa la tano. Kitabu kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa Uraia na Maadili wa mwaka 2016.
Kitabu kimezingatia mwenendo na matarajio ya nchi yetu ya Tanzania katika kukujengea uwezo wa kujipenda na kuwapenda watu wengine, kujivunia shule yako, pamoja na kuipenda nchi yako. Pia, utajifunza muundo wa uongozi serikalini, kujijali na kuwajali watu wengine, kuithamini jamii, kulinda rasilimali na maslahi ya nchi. Aidha, utajifunza namna ya kusimamia majukumu na mambo yanayoonesha tabia ya uvumilivu. Vilevile, maudhui ya kitabu hiki yatakujenga kufikia malengo, tabia ya uadilifu, kusimamia misingi ya demokrasia na kujenga ari ya kudumisha amani katika nchi. Kadhalika, maudhui ya kitabu hiki yatakuwezesha kutambua ushirikiano wa Tanzania na mataifa mengine.
Kitabu hiki kina sura kumi na tatu na kila sura imeundwa na vipengele kadhaa. Aidha, baadhi ya matini ya sura za kitabu hiki yamejengwa kwa visa, habari, mazungumzo, nyimbo, mashairi, ngonjera, michoro na picha. Kila sura ina mazoezi na kazi ya kufanya. Vilevile, ufafanuzi wa msamiati umetolewa mwishoni mwa kila sura ili kukusaidia kuelewa kwa urahisi zaidi umahiri unaohusika
read less