Product description
Historia ya maisha ya Siti Binti Saad kama yalivyosawiriwa na Shaaban Robert na Nasra Mohamed Hilal, na sasa, katika tamthiliya hii ya kihistoria, itamfunulia msomaji wasifu na safari ya maisha ya mwanamama huyu. Katika historia ya safari ya Siti Bin
..
read more
Historia ya maisha ya Siti Binti Saad kama yalivyosawiriwa na Shaaban Robert na Nasra Mohamed Hilal, na sasa, katika tamthiliya hii ya kihistoria, itamfunulia msomaji wasifu na safari ya maisha ya mwanamama huyu. Katika historia ya safari ya Siti Bint Saad, msomaji atajifunza: Kwamba, ushindi maishani unawezekana hata kama umetoka katika familia maskini kiasi gani. Kwamba, ili kuwa nyota katika fani au karama yako, uvivu hauna nafasi bali juhudi na kufanya kazi usiku na mchana. Kwamba, katika safari yako ya kufikia kilele cha mafanikio utapambana na ‘marafiki’ waliojaa gele, tadi, inda, fitina, majungu na vikwazo vya kila aina. Yote haya yalimpata Siti, ila alipambana hadi akaibuka kidedea. Kwamba, fani na kipaji chako si kwa faida yako binafsi pekee, bali zaidi ni kwa jamii yako. Na kweli, nyimbo za mwanaharakati huyu zililenga kuwatetea wanyonge ikiwa ni pamoja na kukemea ukandamizaji na udhalilishaji wa mwanamke. Alikemea upindishaji wa sheria uliofanywa na matajiri kupitia hongo; ikiwa ni pamoja na wizi uliofanywa na wafanyakazi wa serikali maofisini na viwandani.
read less