Tab Article
ADILI NA NDUGUZE
Hii ni hadithi fupi inayohusu maisha ya kawaida ya binadamu. Mwandishi anajadili dhana ya upendo kama kiini cha ura ki, mapatano, msamaha na wokovu dhidi ya madhila ya binadamu wenye wivu, chuki na mabaya mengine. Mhusika mkuu, Adili, alikuwa adili kwelikweli. Ndugu zake, Hasidi na Mwivu wanapanga kumwangamiza ili kurithi mali zake na mchumba wake. Ubaya unawarudia wao lakini wema wa Adili unaleta wokovu kwa wote watatu.
UTUBORA MKULIMA
Utubora ni kijana jasiri, mvumilivu, mwaminifu, mkweli na mwenye msimamo katika maamuzi yake. Mwandishi amemchora mhusika huyu kama kielelezo cha vijana wengi wanaokumbana na misukosuko ya maisha. Mathalan, anashindwa kuendelea na masomo baada ya baba yake kufariki gha a. Hata hivyo, Mungu hamtupi mja wake. Baadaye, anapata kazi ya ukarani katika kampuni ya tajiri Ahmed na kuwa maarufu kuliko watu wote kwenye ofisi hiyo. Licha ya kulipwa mshahara mkubwa, anaacha kazi na kuingia katika kilimo anachoamini kitamuinua zaidi. Je, ataweza?
SIKU YA WATENZI WOTE
Hii ni riwaya inayojadili uhusiano baina ya wanadamu na baina ya wanadamu na Mungu. Ni riwaya inayozungukia kipindi cha mabadiliko katika nchi ya Tanganyika mara tu baada ya uhuru katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni, hasa kisiasa. Tabaka la wenye nacho linaendeleza dhuluma, u sadi, ukatili na uonevu huku likiwaacha watu wa tabaka la chini katika njaa, umasikini, makazi duni na kukata tamaa. Kupitia wahusika kama vile Akili na Ayubu, mwandishi anabainisha kuwa suluhisho la matatizo ya jamii linaweza kupatikana kupitia wanajamii wenyewe.