Product description
KUSADIKIKA
Kusadikika ni riwaya fupi inayozungumzia athari za ujinga, ubinafsi na tamaa za viongozi katika jamii. Katika riwaya hii, viongozi wa nchi ya Kusadikika wamepewa mamlaka makubwa kiasi kwamba chochote wakisemacho ni amri. Jambo hili linaku
..
read more
KUSADIKIKA
Kusadikika ni riwaya fupi inayozungumzia athari za ujinga, ubinafsi na tamaa za viongozi katika jamii. Katika riwaya hii, viongozi wa nchi ya Kusadikika wamepewa mamlaka makubwa kiasi kwamba chochote wakisemacho ni amri. Jambo hili linakuwa hatari sana hasa pale kiongozi akiwa ni mtu aliyejaa chuki na wivu. Matokeo yake, raia ambao ni watu wasio na vyeo, wanapata shida kubwa sana katika nchi hii. Riwaya hii kogwe imejaa elimu na maarifa muhimu kwa jamii.
KUFIKIRIKA
Ku kirika ni riwaya fupi inayotumia mandhari ya ku kirika lakini maudhui yake yanasadifu maisha ya jamii kwa sehemu kubwa. Kwa kawaida ndoa katika jamii nyingi hazipo kwa ajili ya mume na mke kuishi pamoja tu bali pia kupata watoto. Watoto ndiyo furaha na faraja kuu ya wanandoa. Kutokana na imani hiyo, ndoa ya mfalme na malkia wa Ku kirika inagubikwa na wingu la huzuni kuu kwa kuandamwa na ugumba na utasa. Je, waganga mbalimbali walioitwa wataweza kupata suluhisho la tatizo hili?
MASOMO YENYE ADILI
Kitabu hiki kimekusanya mambo mengi ya hekima. Ni kitabu ambacho kimejaa hadithi fupi zenye maonyo, ushauri, maelekezo na maadili mbalimbali yahusuyo maisha. Yapo mashairi yenye wingi wa hekima ndani yake ambayo sambamba na hadithi fupi yanafanya kazi ya kuadilisha jamii katika nyanja zote za maisha. Kitabu hiki ni darasa tosha na daraja bora la kupitishia maarifa kutoka kwa mwandishi kwenda kwa wasomaji.
read less