Product description
Alizeti ni moja ya mazao makuu ya biashara yanayostawishwa hapa nchini. Mbegu zake hutoa mafuta asilimia 35-45 na mashudu yake hutumika kulisha mifugo. Mafuta daraja la kwanza hutumika kupikia chakula cha binadamu na ya daraja la pili hutumika viwand
..
read more
Alizeti ni moja ya mazao makuu ya biashara yanayostawishwa hapa nchini. Mbegu zake hutoa mafuta asilimia 35-45 na mashudu yake hutumika kulisha mifugo. Mafuta daraja la kwanza hutumika kupikia chakula cha binadamu na ya daraja la pili hutumika viwandani kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile sabuni, rangi, vipodozi mbalimbali n.k. Mafuta ya kupikia ya alizeti ni mazuri sana kwa afya na yanapendwa sana na walaji nchini na nje ya nchi.
Hapa nchini bado wapo wakulima wengi ambao bado wanalistawisha bila kuzingatia kanuni za kilimobiashara. Mavuno wanayoyaambulia ni magunia tatu (kilogramu 180) hadi magunia 5 (kilogramu 300). Lakini, mkulima akiendesha kilimobiashara, kwa kutekeleza kanuni zote, hupata magunia 20 (kilogramu 1,200) hadi magunia 27 (kilogramu 1,620).
Bei nzuri ya mbegu huanzia sh. 500/= hadi sh. 1,000/= kwa kilo moja kwa kutegemea hali ya soko ndani na nje ya nchi. Zidisha kilo ulizozipata na bei iliyopo na utaona jinsi kilimo cha zao hili kinavyoweza kutokomeza umaskini wa wakulima. Bei ya mashudu huanzia sh. 250/= hadi sh. 500 kwa kilogramu moja. Kwa hakika, wadau wote: wakulima, maduka yanayouza zana na pembejeo, maofisa ugani, wanunuzi wa alizeti, viwanda vya kusindika mbegu n.k. wana mchango mkubwa katika kuanzisha na kuendeleza kilimobiashara cha alizeti nchini. Basi, watimize wajibu wao.
Mwandishi wa kitabu hiki ameeleza kanuni za kilimobiashara cha alizeti. Wakulima wa alizeti wapya na wa zamani, viongozi na maofisa kilimo, wanashauriwa kukisoma na kuzingatia yaliyomo kwa faida yao na ya taifa zima.
read less