Product description
Kitabu hiki kimeandikwa ili kiwasaidie Wakulima, Maofisa Ugani, Wanafunzi na Wanavyuo kuanzisha aina mpya ya kilimo, yaani, Ustawishaji wa Mbogamboga. Kutokana na wingiwa aina za mbogamboga zilizopo, kitabu kimeandikwa kwamuhtasari. Hata hivyo, hatuk
..
read more
Kitabu hiki kimeandikwa ili kiwasaidie Wakulima, Maofisa Ugani, Wanafunzi na Wanavyuo kuanzisha aina mpya ya kilimo, yaani, Ustawishaji wa Mbogamboga. Kutokana na wingiwa aina za mbogamboga zilizopo, kitabu kimeandikwa kwamuhtasari. Hata hivyo, hatukuweza kueleza kilimo cha aina zote za mboga. Zipo chache ambazo zimeachwa. Kitabu kimegawanywa katika sehemu mbili: Sehemu ya Kwanza inaeleza Misingi ya Kustawisha Mbogamboga. Sehemu ya Pili inaeleza Ustawishaji wa Aina mbalimbali za Mbogamboga. Kila sehemu imegawanywa katika sura kadhaa. Sehemu ya Kwanza ina sura tisa na Sehemu ya Pili ina sura sita. Mwishoni mwa kila sura yapo Maswali ya kumsaidia msomaji ajipime kama ameielewa vizuri sura hiyo. Kuna nyongeza mbili. Nyongeza ya Kwanza ni Orodha ya Viuatilifu (dawa) vya kuua wadudu waharibifu wa mimea ya mazao na maelezo ya namna vinavyoua. Nyongeza ya Pili inaeleza Kanuni za Kiusalama za Kuhifadhi na kutumia Viuatilifu vya kudhibiti Magonjwa na Wadudu wa mimea. Ustawishaji wa Mbogamboga ni aina ya kilimo inayoweza kumwingizia mkulima mapato makubwa ndani ya kipindi kifupi.
Natumaini kuwa kitabu hiki kitasaidia kufanya lishe ya wananchi kuwa nzuri zaidi.
Aidha, kitasaidia kuongeza mapato ya wakulima na ya taifa.
read less