Tab Article
A. Outline of the book
The book, written in Kiswahili, has the following 5 chapters:
1. Asili, Maana, Umbile, Mazingira, Maisha, aina, Makundi na Faida za Uyoga.
2. Misingi mikuu ya kilimo cha Uyoga.
3. Kanuni na Mahitaji ya kilimo cha Uyoga.
4. Visumbufu vya Uyoga.
5. Uvunaji, Hifadhi, Ufungashaji na Mapishi ya Uyoga
Brief Summary
The book is about How to Grow Mushrooms.
B. Maelezo mafupi ya kitabu:
Uyoga ni zao la viumbehai viitwavyo kuvu. Kwa watu wengi hapa nchini Uyoga unaofahamika ni ule unaookotwa au unaoonekana ukiota porini au kwenye vichuguu wakati wa msimu wa mvua. Ukiwaeleza kuwa uyoga hustawishwa kama ilivyo kwa mazao mengine, hawakuelewi! Ukiwaeleza kuwa uyoga huweza kumwingizia mkulima fedha nyingi, pia hawakuelewi. Lakini, hawana kosa. Kilimo cha Uyoga nchini ni kipya na ni kichanga. Kwa wale wakulima wachache walioanza kustawisha Uyoga, bado mavuno ni kidogo. Hii imetokana na wao kutokuwa na maarifa ya kilimo bora cha zao hili. Lengo la kitabu hiki ni kuwawezesha wafanikishe kilimo hiki. Kitabu hiki kinaeleza namna ya kustawisha Uyoga.