Tab Article
Kitabu cha Kiswahili Kidato cha nne kwa shule za sekondari Tanzania kimeandikwa kwa kutumia silabasi mpya ya mwaka 2005 badala ya ile ya mwaka 1997. Hiki ni kitabu cha nne kuandikwa kwa kuzingatia kanuni za Lugha zinazomfikirisha mwanafunzi na pia kumpa stadi za kuitumia lugha katika mazingira mbalimbali. Vitabu vingi vya wanafunzi vya Kiswahili vimejaa sarufi kavukavu hivyo kupoteza ladha kwa msomaji. Wanafunzi na walimu watakifurahia kitabu hiki ambacho kimegusa mada zote za Kidato cha Kwanza.
Dr. Michael Kadeghe ni Mhadhiri wa Lugha wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anacho Cheti na Stashahada ya Lugha ya Kiswahili; anayo Shahada ya Ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BED); anayo Shahada ya Uzamili katika Lugha (Masters in Linguistics) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; anayo Shahada ya juu ya Udaktari wa Falsafa katika Lugha (PhD in Linguistics) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na vyeti kadhaa vya mafunzo kutoka Uingereza, Malesia na Marekani.