Tab Article
Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kidato cha Pili; ni kitabu cha kwanza na kipya kabisa kuandikwa hapa nchini ili kukidhi haja ya silabasi iliyopo. Kimekusudiwa kiwafae wanafunzi wa kidato cha pili. .. Kitawafanya wanafunzi na walimu wao kulifurahia somo la Kiswahili kwa kuwa ~ kimekusanya mad a zote zinazofundishwa katika kiwango hiki. Hiki ni kitabu .cha lazima kwa kila mwanafunzi wa kidato cha pili hapa nchini Tanzania.
Godfrey Rutta Bukagile ni msomi, mhariri, mwalimu na mwandishi wa vitabu vya taaluma hapa nchini Tanzania. alizaliwa kijijini Kikukwe, kata ya Kanyigo, wilaya ya Bukoba vijijini mkoani Kagera. Ana stashahada ya ualimu kutoka Chuo cha Ualimu Korogwe na Shahada ya Ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Oar es Salaam. Kwa sasa ni mwalimu wa Midlands High School, jijini Oar es Salaam .
.
J.A. Masebo alizaliwa katika kijiji cha Kafule, Ileje mkoani Mbeya. Alipata elimu ya msingi katika shule ya Kafule (lsoko). Elimu ya Sekondari aliipata katika shule ya Kafule na Sengerema. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Oar es Salaam kusomea B.A. (Ed); ambapo alihitimu na kutunukiwa shahada ya B.A. (Ed) (Hons). Shule alizowahi kufundisha Kiswahili ni Kafule sekondari, Mkwawa sekondari, Makongo sekondari na Midlands sekondari. Ndugu Masebo ni mwandishi wa vitabu vya somo la Kiswahili (Fasihi na Isimu) katika viwango mbalimbali vya elimu hapa nchini.