Product description
Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kidato cha Tatu; ni kitabu kinaehokidhi haja ya silabasi iliyopo. Kimekusudiwa kiwafae walimu na wanafunzi wa kidato cha tatu. Kitabu hiki kimejadili mada zote kwa uyakinifu na utoshelevu ,kama ambavyo muhtasari unavy
..
read more
Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kidato cha Tatu; ni kitabu kinaehokidhi haja ya silabasi iliyopo. Kimekusudiwa kiwafae walimu na wanafunzi wa kidato cha tatu. Kitabu hiki kimejadili mada zote kwa uyakinifu na utoshelevu ,kama ambavyo muhtasari unavyoongoza. Ni matarajio ya waandishi kuwa kitabu hiki kitaziba mapengo yaliyojitokeza baada ya mabadiliko ya lazima ya muhtasari.
Greyson Godfrey Mhilu alizaliwa mkoani Dodoma na kusoma katika shule za msingi Nghwenda na Mkoyo. Alijiunga Bihawana na Mkwawa kwa elimu ya sekondari. Alihitimu shahada ya kwanza (Shahada ya Elimu na Sanaa) mwaka 2003 katika Chuo Kikuu eha Dar-es- Salaam. Alijiunga na Chuo Kikuu eha Stetson kiliehopo jimbo la Florida, Marekani kama mhadhiri kupitia Fulbright.
J.A. Masebo alizaliwa katika kijiji eha Kafule, Ileje mkoani Mbeya. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Kafule (Isoko). Alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Kafule na Sengerema. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea shahada ya Elimu na Sanaa. Shule alizowahi kufundisha Kiswahili ni Kafule Sekondari, Mkwawa Sekondari, Makongo Sekondari na Midlands Sekondari. Ndugu Masebo ni mwandishi wa vitabu vya somo la Kiswahili (Fasihi na Isimu) katika viwango mbalimbali vya elimu hapa nehini.
read less