Categories: Autobiography

Laiti Ningelijua

  • ISBN: 9789987971091
  • Number of pages: 141 pages
  • Product format: Paperback
  • Publisher: UWARID
  • Year published: 2020
  • Availability: In stock
10,000 TZS

Product description

Watanzania waliokuwa na akili za kujitambua kwenye miaka ya 80 na 90 watakubali kuwa hapajawahi kutokea jarida la vikaragosi, riwaya na burudani lililopendwa zaidi nchini kama SANI. Ila ni wachache wanaojua kuwa jarida lile ni zao la watunzi wawili m

Qty

Tab Article

Watanzania waliokuwa na akili za kujitambua kwenye miaka ya 80 na 90 watakubali kuwa hapajawahi kutokea jarida la vikaragosi, riwaya na burudani lililopendwa zaidi nchini kama SANI. Ila ni wachache wanaojua kuwa jarida lile ni zao la watunzi wawili mahiri nchini, SAlim Bawji (marehemu) na NIcco ye Mbajo; na k .. wamba ni muunganiko wa herufi mbili za mwanzo za majina yao ndio unaounda jina la jarida hili pendwa na maarufu zaidi nchini, SAN!.
LAITI NINGELIJUA ni kitabu kinachofuatilia maisha ya mmoja wa waasisi wa jarida lile, mzee Nicco ye Mbajo - mchoraji, mtunzi, msanii, na mwalimu wa kwaya - tangu uzawa wake hadi h:ii leo, kwa maneno yake mwenyewe. Ni mtiririko wa matukio ya kufurahisha, kushangaza, kuhuzunisha na hata kuduwaza - kiasi cha kukufanya ujiulize iwapo ni kisa cha kweli ama cha kubuni? Hii ni tawasifu adhimu kuhusu maisha ya msanii huyu mwenye vipaji vingi aliyeacha athari kubwa kwenye maisha ya Watanzania wengi, ambaye hata hivyo anaishia kwenye majuto yanayozaa mjukuu aliyetawala jina la kitabu hiki. .. LA TI NINGELIJUA!

0 reviews for Laiti Ningelijua

Add a review

Your Rating