Tab Article
Makuadi wa Soko Huria ni hadithi ya Kihistoria yenye ukweli unaodhihirika leo.Inatoa taswira ya mapambano ya Watanzania katika kujipatia uhuru na amani ya kweli.Mapambano dhidi ya ukoloni na baadaye dhidi ya baadhi ya watu wao walioteka nyara uhuru wa wengi na kushirikiana na wageni kupora rasilimali ya nchi kwa kisingizio cha soko huria.Hadithi inaweka bayana uozo na udhalimu uliojificha katika mfumo wa soko huriatamaa ya pesa na nguvu za kiuchumi,ubinafsi na ukandamizaji.Pia ni hadithi ya matumaini.Inatuonyesha jinsi watu wasivyokubali kukandamizwa,wasivyokata tamaa.Makuadi wa Soko Huria inatukumbusha kwamba utu wa binadamu hauvunjwi kwa pesa wala kwa mabavu.