Product description
Natumaini hakuna atakayepingana na ukweli kwamba kuzaa ni kazi rahisi zaidi ukilinganisha na kulea. Kwa uzoefu wa miaka kadhaa sasa kwenye tasnia ya ushauri wa kisaikolojia “counseling†nimegundua kuwa wazazi wengi sana wanajua vizuri kuz
..
read more
Natumaini hakuna atakayepingana na ukweli kwamba kuzaa ni kazi rahisi zaidi ukilinganisha na kulea. Kwa uzoefu wa miaka kadhaa sasa kwenye tasnia ya ushauri wa kisaikolojia “counseling†nimegundua kuwa wazazi wengi sana wanajua vizuri kuzaa lakini suala la kulea ni changamoto kwao. Wengi hutupiana jukumu hili baina ya wao kwa wao na wengine huwatupia ndugu zao, wazazi wao “babu na bibi†au walimu mashuleni. Utakubaliana na mimi kwamba leo kuna ongezeko kubwa sana la watoto wadogo sana kupelekwa shule za bweni, pamoja na kwamba sababu zipo nyingi na tofauti lakini ukweli ni kwamba wazazi wengine wanatumia fursa hiyo kukwepa jukumu lao la malezi. Jamii ya sasa inachangamoto nyingi na nyingine hazikwepeki, yapo maendeleo ya kiteknolojia, kiviwanda, kiuchumi na kijamii. Maendeleo haya tutake au tusitake yanaathiri eneo la familia na malezi kwa kiasi kikubwa sana. Leo tunashuhudia ongezeko kubwa sana la wazazi wanaolewa watoto bila mzazi mwenza “single parentingâ€, changamoto hii imeambatana na athari nyingi sana kwa watoto hawa bila kusahau changamoto za kihisia kwa wazazi husika. Mambo haya yote yamenifanya kuandika kitabu hiki ili kumsaidia mzazi, mlezi na yeyote mwenye mawazo ya kujakuwa mzazi huko mbeleni ili kuweza kupata ujuzi na uelewa wa mambo
read less