Product description
Penina Muhando (Pia Penina Mlama) ni mwandishi mbobevu na mwanazuoni wa Kiswahili hususan katika utanzu wa tamthiliya. Ameandika tamthiliya kama vile Heshima Yangu (1974), Pambo (1975), Lina Ubani (1984) na Mitumba Ndui (1989). Pia amewahi kuhudumu k
..
read more
Penina Muhando (Pia Penina Mlama) ni mwandishi mbobevu na mwanazuoni wa Kiswahili hususan katika utanzu wa tamthiliya. Ameandika tamthiliya kama vile Heshima Yangu (1974), Pambo (1975), Lina Ubani (1984) na Mitumba Ndui (1989). Pia amewahi kuhudumu kama Profesa Mshiriki kwenye Idara ya Sanaa na Maonyesho katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; kama mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Forum for African Women Educationists (FAWE). Profesa Mhando pia ni mwanzilishi mwenza wa TUSEME – mradi wa
kuwasaidia wasichana kutambua na kutatua changamoto zinazowazuia kupiga hatua kielimu na kijamii na sasa ni mgoda wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere (2021 ).Nguzo Mama ni tamthiliya inayozungumzia changamoto zinazowakabili wanawake kwenye jamii ambazo zimekuwa minyororo inayowazuia kukia kilele cha ukombozi wao.
Tunaona nguzo kubwa, nzito imelala chini. Inatakiwa kunyanyuliwa ili isimame wima. Akina mama wengi wanajaribu kuinyanyua, lakini kila wanapoanza, linatokea hili au lile. Hatimaye mmoja baada ya mwingine wanatelekeza jukumu hilo. Je, nini kifanyike ili nguzo hii inyanyuke? Katika tamthiliya hii, mwandishi ametumia fani ya fasihi simulizi, si tu kukisha ujumbe, bali pia ameufanya mchezo kuwa wa kuvutia na kusisimua.
read less