Categories: Popular books

Takadini

  • ISBN: 9789987602193
  • Product format: Paperback
  • Author: MATHEW BOOKSTORE
  • Publisher: APE Network
  • Year published: 2021
  • Availability: In stock
6,000 TZS

Product description

Riwaya ya kipeke inayovutia hisia, ambayo inasawiri mila na desturi huku ikijikita katika karne ya 19 nchini Zimbabwe. Japokuwa ilikuwa ni mwiko kuruhusu kuwepo kwa mazeruzeru, yaani wakipokonywa maisha yao punde wazaliwapo, mwanamke mmoja jasiri ana

Qty

Tab Article

Riwaya ya kipeke inayovutia hisia, ambayo inasawiri mila na desturi huku ikijikita katika karne ya 19 nchini Zimbabwe. Japokuwa ilikuwa ni mwiko kuruhusu kuwepo kwa mazeruzeru, yaani wakipokonywa maisha yao punde wazaliwapo, mwanamke mmoja jasiri anamtorosha takadini, mwanawe aliye zeruzeru ili kuyanusuru maisha yake.

Lakini, hata katika nchi wanayokimbilia, jamii inavutana sana, wengi wakiamini kuwa kuwepo kwa Takadini na mama yake kungewaletea mkosi. Hata hivyo, baadhi ya wazee wanatumia busara kuupoza mgogoro huo, japokuwa kwa vikwazo vingi.

Takadini alikuwa sope yaani zeruzeru na hatimaye alipata ulemavu, akatengwa na watoto wenzake huku wengine wakimkejeli. katikati ya unyonge na mashaka, Takadini na mama yake wanafarijika kwa mapenzi wanayopewa na Baba Chivero, mganga mshauri ambaye kabla hajafa anamfundisha Takadini tiba mbalimbali. Hata Takadini anapoibuka kuwa mpigaji mbira hodari, hatimaye jamii inaanza kuvutiwa naye. Akatokea msichana akampenda, wakaoana na wakapata mtoto asiye sope. Kumbe ulemavu wake na uzeruzeru wake, havikumzuia kuyatenda yale wafanyayo binaadamu wengine. Je, taswira hiyo ya mila dhidi ya masope ingepokewaje na jamii ya mama yake Takadinii pindi watakaporeje?

0 reviews for Takadini

Add a review

Your Rating