Categories: Business

Uhuru Wa Mahakama

35,000 TZS

Product description

Jaji Barnabas A. Samatta, alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka 2000 hadi 2007. Huko nyuma, 1984-1987, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe. Yeye ni mjumbe mwanzilishi wa Judicial Integrity Group (Kikundi cha Uadilifu wa Mahakama), chombo huru cha

Qty

Tab Article

Jaji Barnabas A. Samatta, alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka 2000 hadi 2007. Huko nyuma, 1984-1987, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe. Yeye ni mjumbe mwanzilishi wa Judicial Integrity Group (Kikundi cha Uadilifu wa Mahakama), chombo huru cha kimataifa kinacho jishughulisha na ukuzaji wa uadilifu wa mahakama duniani na ambacho kilitunga Kanuni za Bangalore za Mwenendo wa Mahakama. Kwa wakati huu, yeye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bodi ya Kampuni ya Earth, Energy and Environment Mediation Limited yenye makao makuu yake London, Uingereza, ambayo inashughulikia njia bora za kuzuia au kutatua migogoro barani Afrika inayohusiana na ardhi, mafuta, madini, maji au mazingira. Vilevile, Jaji Samatta ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe. Katika baadhi ya hukumu, makala na hotuba zake amesisitiza sana juu ya umuhimu wa uhuru wa mahakama, usawa mbele ya sheria na upatikanaji wa haki kwa unafuu na wepesi kwa kila mtu katika jamii. Katika kitabu hiki, anazungumzia kwa ufasaha, lakini kwa lugha nyepesi kuelewa, na kwa namna isiyomchosha msomaji, masuala mengi muhimu sana katika uwanja wa utoaji wa haki. Miongoni mwake ni uhuru wa mahakama; rushwa; ugumu wa kazi na maisha ya jaji; mikwaruzano baina ya mihimili ya dola na utumiaji wa kiuonevu wa mamlaka ya dola. Hiki ni kitabu kwa mwanasheria na kwa mlei. Ni kitabu kwa mtawala na mtawaliwa. Kwa kweli, ni kitabu kwa kila mtu.

0 reviews for Uhuru Wa Mahakama

Add a review

Your Rating