Categories: Literature

Vipande vya maisha vilivyopotea

  • ISBN: 9789976892345
  • Product format: Paperback
  • Author: Lorna Dadi
  • Publisher: APE Network
  • Availability: In stock
15,000 TZS

Product description

Ilikuwa ni mwaka mmoja tangu nikutane na Bahati na Neema, niliposikia simu ya mezani ya ofisini kwangu ikiita. Nilipoinua mkono wa simu nilishtuka kugundua kwamba sauti ya upande wa pili ilikuwa ni ya Rachel, mke wa marehemu Joshua Halimeshi. Nilisht

Qty

Tab Article

Ilikuwa ni mwaka mmoja tangu nikutane na Bahati na Neema, niliposikia simu ya mezani ya ofisini kwangu ikiita. Nilipoinua mkono wa simu nilishtuka kugundua kwamba sauti ya upande wa pili ilikuwa ni ya Rachel, mke wa marehemu Joshua Halimeshi. Nilishtuka kwani haikuwa kawaida ya Rachel kunipigia simu. Mara ya mwisho kuongea naye ilikuwa takribani miaka mitatu kabla ambapo alikuja ofisini kwangu kuulizia deni la R&J Investments. Na siku hiyo alilipa ada ya miaka kumi mbele, zaidi ya deni walilokuwa wanadaiwa.nalo.
“Ndiyo Rachel, habari za siku nyingi?”
“Nzuri tu. Nina shida ya kuonana na wewe ofisini kwako, sijui naweza kuja lini na wakati gani?” Aliuliza Rachel
“Nipo hadi saa sita na nusu, kisha nitakuwepo tena kuanzia saa nane na robo hadi saa kumi na robo jioni.” Nilimweleza.
“Nakuja kabla ya saa sita”
“Karibu Rachel.”
Rachel alikuja ofisini kwangu kwa kutumia gari lake. Alifika saa tano asubuhi. Katika kipindi cha miaka saba ya ujane wake, hakuna siku niliyomuona Rachel amependeza kama siku hiyo. Nilishitushwa sana na uzuri wa Rachel.
Rachel aliniambia kwamba ana maongezi mazito sana yanayohitaji msaada wa kitaalamu. Na alisisitiza kutokana na unyeti wa maongezi hayo, asingependa tuyaongelee pale ofisini na asingependa tuchukue muda mrefu kabla hatujayaongea. Nilimuomba Rachel kwamba, jioni hiyo niende na binti zangu wawili kwani msaidizi wangu wa kazi za nyumbani alikuwa anaumwa. Rachel alikubali. Rachel alishtuka kusikia nina watoto kwani alichojua yeye ni kwamba mke wangu na mtoto walifariki wakati anajifungua. Pamoja na kumbukumbu hiyo, Rachel hakutaka kunihoji sana. Tulikubaliana kwamba mimi ningeenda nyumbani kwa Rachel saa kumi na mbili na nusu jioni ya siku hiyo.
Rachel alimuarifu msaidizi wa wake wa kazi za nyumbani, Kage, juu ya ugeni huo siku hiyo na kwa hiyo alitayarisha vyote alivyopaswa kutayarisha. Muda ulipofika niliingia nyumbani kwa Rachel nikiwa na wanangu. Rachel alishtuka sana alipowaona Neema na Bahati, alihisi maumivu ya siku mwanaye alipotekwa. Alikuwa kama amechanganyikiwa kwa dakika cada. Kage kwa kujua hilo, alimshika Rachel akampeleka kwenye bustani kisha akatukaribisha ndani. Kage aliporudi aliniambia,
“Samahani kaka, dada Rachel bado ana tatizo akiona watoto wa kike ambao anaamini ni umri ambao angekuwa nao Judy; huwa anashtuka sana”.

0 reviews for Vipande vya maisha vilivyopotea

Add a review

Your Rating