Product description
KOJA LA LUGHA
Uhodari na utunzi mahiri wa Shaaban Robert unadhihirishwa katika kazi yake hii ya Koja la Lugha. Mashairi yaliyosukwa kwa ustadi na kubeba tunu za jamii yamekusanywa na kuunda kitabu hiki. Jamii ya Afrika Mashariki ni hadhira lengwa kw
..
read more
KOJA LA LUGHA
Uhodari na utunzi mahiri wa Shaaban Robert unadhihirishwa katika kazi yake hii ya Koja la Lugha. Mashairi yaliyosukwa kwa ustadi na kubeba tunu za jamii yamekusanywa na kuunda kitabu hiki. Jamii ya Afrika Mashariki ni hadhira lengwa kwa namna ya ajabu ya mfanano kati ya yanayozungumziwa na yaliyopo leo hii. Ukongwe si nongwa kwani diwani hii ni kioo cha jamii hata hivi leo.
KIELEZO CHA FASILI
Elimu iliyokita mizizi imara juu ya masuala mbalimbali ya jamii kama vile ndoa, maonyo, heshima na furaha inafafanuliwa katika kazi hii. Si yote ni matamu na si vyote ni machungu bali ni mchanganyiko wa vyote vinavyoifanya jamii kuitwa jamii. Mwandishi anayaelezea mambo haya ya jamii kwa njia ya mashairi na tenzi, kisha anatoa fasili ya kila shairi au utenzi kwa lugha ya kawaida. Ungana na Shaaban Robert katika kitabu hiki kinachogusia mambo mengi ya msingi sana kwa ustawi wa mwanadamu na mazingira yake.
ALMASI ZA AFRIKA
Huu ni mkusanyiko wa mashairi, riwaya na tenzi nyingi za thamani, zenye wingi wa hekima na maadili mema kuhusu maisha ya binadamu. Mwandishi anayatazama maisha katika nyanja zote - kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Kwa jumla ameyatafakari maisha na kuyaona kuwa yamejaa mambo mengi, mema na mabaya. Hata hivyo, ni wale tu wenye hekima ya maisha ndio wanaweza kupenya katikati ya msitu wa maisha kwa usalama na fanaka. Soma kitabu hiki uvune hekima hizo.
read less