Product description
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Hisabati, kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba. Uandishi wa kitabu hiki umezingatia mahitaji yako katika kukuza na kuend
..
read more
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Hisabati, kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba. Uandishi wa kitabu hiki umezingatia mahitaji yako katika kukuza na kuendeleza umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK). Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo la Hisabati wa mwaka 2019 uliotolewa na wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. Kitabu kina sura 13 ambazo ni: Namba nzima, Kujumlisha na kutoa namba nzima, Kuzidisha namba nzima, Kugawanya namba nzima, MAGAZIJUTO, Uwiano, Vipeo na vipeuo vyapili vya namba, Sehemu na desimali, Aljebra, Mwendokasi, Kanuni ya Pythagoras, Hesabu za biashara, na Takwimu. Maudhui ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya mifano, mazoezi, shughuli, kazi mradi na picha zenye mvuto ambazo zinachochea ujenzi wa ujuzi na maarifa yaliyokusudiwa. Hivyo basi, unapaswa kufanya kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi nyingine utakazopewa na mwalimu.
read less