Tab Article
JlZATITI KATIKA KISWAHILI ni kitabu kilichoandaliwa mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la V, VI na VII, pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo. Aidha, kitabu hiki pia kinafaa sana kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kufuatilia na kuwasaidia watoto wao kitaaluma .
JlZATITI KATIKA KISWAHILI kimetungwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa somo la Kiswahili Tanzania. Kitabu hiki kimetungwa ili kiwe msaada kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi, ambao kwa muda rnrefu wamekuwa wakipata ugumu katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili; hali ambayo imepelekea
wanafunzi kupata matokeo yasiyoridhisha katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kinyume kabisa na matarajio ya wengi.
Kitabu hiki kina mazoezi ya kutosha ambayo yametungwa kutokana na mada ndogo na madhumuni mahsusi na hivyo kuwawezesha walimu kutoa mazoezi mengi na wanafunzi kufanya mazoezi hayo kwa kila mada ndogo na madhumuni maalumu. Pia methali, nahau na vitendawili vimewekwa vingi vya kutosha ili kurahisisha zoezi zima la kujifunza na ufundishaji. Majibu ya maswali yote yamepitiwa na kuhakikiwa kwa umakini wa hali ya juu.
Kitabu hiki cha JlZATITI KATIKA KISWAHILI ambacho kila mwanafunzi na kila mwalimu anatakiwa kuwa nacho kikitumika ipasavyo:
⦁ kitamwezesha mwanafunzi kufanya kwa ufanisi majaribio na mitihani mbalimbali ya somo la Kiswahili na hatimaye kuweza kufaulu vizuri mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
⦁ kitamwezesha mwalimu kumudu kufundisha somo la Kiswahili kwa ufanisi zaidi.
⦁ kitamwezesha mwanafunzi kuongeza ari ya kujifunza somo la Kiswahili na hatimaye kuweza kuimudu vyema lugha yetu adhimu ya Taifa.
⦁ kitaboresha ufundishaji wa mwalimu.
⦁ kitawawezesha walimu na wanafunzi kupunguza muda wa kusoma vitabu vingi tofauti tofauti kwa ajili ya kuandaa somo ama kujifunza.
Mtunzi wa kitabu hiki amewashirikisha wataalamu wa somo la Kiswahili ambao wamefundisha somo hili katika shule mbalimbali kwa mafanikio makubwa. Aidha, kwa nyakati tofauti, wataalamu hawa wameshiriki katika mafunzo mbalimbali ya ufundishaji bora wa somo hili ikiwemo pia katika tathmini zinazohusiana na maendeleo na changamoto za ufundishaji wa somo kwa ujumla.
Pia, wataalamu hawa, wamewahi kushiriki katika warsha za mabadiliko ya mitaala ya shule za msingi katika miaka ya 1996,2000 na 2005.
Pamoja na kushiriki katika tathmini ya kujua nini chanzo cha matokeo yasiyoridhisha ya somo la Kiswahili katika mitihani ya darasa la saba, wataalamu hawa pia wamewahi kushirikishwa katika utungaji wa mitihani mbalimbali.