Categories: Popular books

Jizatiti Katika Maarifa ya Jamii

15,000 TZS

Product description

JIZATITI KATIKA MARIFA YA JAMII ni kitabu kilichoandaliwa mahsusi kwa wanafunzi wa darasa la V, VI na VII, pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo. Aidha, kitabu hiki pia kinafaa sana kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kufuatilia na kuwasaidia

Qty

Tab Article

JIZATITI KATIKA MARIFA YA JAMII ni kitabu kilichoandaliwa mahsusi kwa wanafunzi wa darasa la V, VI na VII, pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo. Aidha, kitabu hiki pia kinafaa sana kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kufuatilia na kuwasaidia watoto wao kitaaluma.
JIZATITI KATIKA MARIFA YA JAMII kimetungwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa masomo ya Uraia, Historia na Jiografia Tanzania. Kitabu hiki kimetungwa ili kiwe msaada kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata ugumu katika ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Maarifa ya Jamii; hali ambayo imepelekea wanafunzi kupata matokeo yasiyoridhisha katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kinyume kabisa na matarajio ya wengi.
Kitabu hiki kina mazoezi ya kutosha ambayo yametungwa kutokana na mada ndogo na madhumuni mahsusi na hivyo kuwawezesha walimu kutoa mazoezi mengi na wanafunzi kufanya mazoezi hayo kwa kila mada ndogo na madhumuni maalumu. Pia maumbo na michoro yote vimechorwa kwa ustadi mkubwa ili kurahisisha zoezi zima la kujifunza na ufundishaji. Majibu ya maswali yote yamepitiwa na kuhakikiwa kwa umakini wa hali ya juu.
Kitabu hiki cha JIZATITI KATIKA MARIFA YA JAMII ambacho kila mwanafunzi na kila mwalimu anatakiwa kuwa nacho kikitumika ipasavyo:
⦁ kitamwezesha mwanafunzi kufanya kwa ufanisi majaribio na mitihani mbalimbali ya Maarifa ya Jamii na hatimaye kuweza kufaulu vizuri mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
⦁ kitamwezesha mwalimu kumudu kufundisha somo la Maarifa ya Jamii kwa ufanisi zaidi.
⦁ kitamwezesha mwanafunzi kuongeza ari ya kujifunza somo la Maarifa ya Jamii.
⦁ kitaboresha ufundishaji wa mwalimu.
⦁ kitawawezesha walimu na wanafunzi kupunguza muda wa kusoma vitabu vingi tofauti tofauti kwa ajili ya kuandaa somo ama kujifunza.
Mtunzi wa kitabu hiki amewashirikisha wataalamu wa masomo ya Maarifa ya Jamii ambao wamefundisha masomo hayo katika shule mbalimbali kwa mafanikio makubwa. Aidha, kwa nyakati tofauti, wataalamu hawa wameshiriki katika mafunzo mbalimbali ya ufundishaji bora wa masomo hayo ikiwemo pia katika tathmini zinazohusiana na maendeleo na changamoto za ufundishaji wa masomo haya kwa ujumla.
Pia, wataalamu hawa, wamewahi kushiriki katika warsha za mabadiliko ya mitaala ya shule za msingi katika miaka ya 1996, 2000 na 2005.
Pamoja na kushiriki katika tathmini ya kujua nini chanzo cha matokeo yasiyoridhisha ya somo la Maarifa ya Jamii katika mitihani ya darasa la saba, wataalamu hawa pia wamewahi kushirikishwa katika utungaji wa mitihani mbalimbali.

0 reviews for Jizatiti Katika Maarifa ya Jamii

Add a review

Your Rating