Product description
Hii ni kamusi bora kabisa ya Kiswahili – Kiingereza yenye zaidi ya vidahizo 9,000 na mifano ya matumizi yake kwa lugha zote mbili. Ina vielelezo zaidi ya 280 vya rangi vinavyoonesha sura halisi za vitu na viumbe. Lugha iliyotumika katika kamusi hii
..
read more
Hii ni kamusi bora kabisa ya Kiswahili – Kiingereza yenye zaidi ya vidahizo 9,000 na mifano ya matumizi yake kwa lugha zote mbili. Ina vielelezo zaidi ya 280 vya rangi vinavyoonesha sura halisi za vitu na viumbe. Lugha iliyotumika katika kamusi hii ni rahisi na hivyo maana na mifano inaeleweka kwa urahisi. Kwa utajiri huu wa maneno, mifano lukuki na mpangilio mufti, kamusi hii ni ya kutegemewa kwa watumiaji wa Kiswahili na Kiingereza.
Sifa nyingine za kamusi hii ni:
• Imehaririwa na kupewa ithibati na Baraza la Kiswahili la Taifa - BAKITA.
• Ina mifano mahususi katika vidahizo vingi inayoonesha matumizi ya neno.
• Ina vidahizo vingi yakiwemo maneno mapya yaliyosanifishwa na BAKITA.
• Ina picha angavu na za kuvutia za vitu na viumbe.
• Imezingatia uchaguzi badili wa tahajia za maneno.
Sifa hizi zinaifanya kamusi hii kuwa rejea muhimu ya tafsiri, ukalimani na matumizi ya jumla.
read less