Product description
Kitabu hiki ni cha nne katika mfululizo wa vitabu vya Kiswahili kilichoandaliwa mahususi kwa ajili ya mwanafunzi wa Darasa la sita. Kitabu kinalenga kukuza uwezo wako wa kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili. Pia, kitabu k
..
read more
Kitabu hiki ni cha nne katika mfululizo wa vitabu vya Kiswahili kilichoandaliwa mahususi kwa ajili ya mwanafunzi wa Darasa la sita. Kitabu kinalenga kukuza uwezo wako wa kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili. Pia, kitabu kimelenga kukuwezesha kutumia msamiati wa lugha ya Kiswahili kwa namna mbalimbali, hivyo, kukujengea uwezo wa kupanga mawazo kwa mpangilio na mtiririko unaotakiwa.
Kitabu kina hadithi, habari, mashairi, ngonjera, igizo, mdahalo na majigambo. Vyote hivyo vitakuwezesha kujifunza kwa ufasaha. Kitabu kimesheheni maswali ya kupima ufahamu na mazoezi mbalimbali yanayojenga ujuzi wako katika somo la Kiswahili.
read less