Tab Article
Kitabu hiki ni cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vitatu vya Stadi za Kazi kimeandaliwa mahususi kwa mwanafunzi wa Darasa la Tano.
Kitabu hiki kitakuza umahiri wa stadi za uchunguzi, ugunduzi na udadisi. Pia, kitasaidia kukuza stadi za ubunifu na uturnia]i wa taarifa za Stadi za Kazi.
Aidha, kitabu kina sura saba zilizoandaliwa kukidhi mahitaji ya muhtasari wa somo. Sura hizo ni: Unadhifu, Upishi, Usanifu wa kazi za sanaa za maonesho, Usanifu wa picha, Ufinyanzi na ususi, Stadi za ujasiriamali na Usimamizi wa fedha.
Mwisho, kitabu hiki kinaelekeza maudhui kwa njia ya habari, picha, kazi za vitendo na mazoezi. Pia, kitamjengea mwanafunzi uwezo kwa kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).