Product description
Kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo wa vitabu vitatu vya somo la Stadi za Kazi kuanzia Darasa la Tano hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba: Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo la Stadi za
..
read more
Kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo wa vitabu vitatu vya somo la Stadi za Kazi kuanzia Darasa la Tano hadi la Saba, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Darasa la Saba: Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo la Stadi za Kazi wa mwaka 2019 uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kitabu hiki kimelenga kukuza umahiri wa stadi za uchunguzi, udadisi, ubunifu, ujasiriamali na stadi za maisha. Aidha, kitabu hiki kina sura 12 ambazo ni: Unadhifu; Utunzaji wa mazingira katika makazi; Upishi; Misingi ya uimbaji; Misingi ya uigizaji; Ufinyanzi; Upigaji picha; Uchapaji kwa njia ya kimia; Uzalishaji wa mazao ya mimea; Uzalishaji wa mazao ya mifugo; Kumlinda mlaji na kuvutia wateja na Huduma za kifedha. Kitabu hiki kinawasilisha maudhui kwa njia ya habari, picha, visamafunzo, kazi za vitendo na mazoezi. Hivyo basi, unapaswa kufanya kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi zingine utakazopewa na mwalimu.
read less