Product description
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu kilichoandaliwa mahususi kwa mwanafunzi wa Darasa la Tano. Kitabu hiki kinalenga kukuendeleza katika kujenga stadi za kuhesabu, kuandika na kusoma huku ukijenga msingi wa Hisabati. Aidha, kitabu hiki
..
read more
Kitabu hiki ni cha tano katika mfululizo wa vitabu kilichoandaliwa mahususi kwa mwanafunzi wa Darasa la Tano. Kitabu hiki kinalenga kukuendeleza katika kujenga stadi za kuhesabu, kuandika na kusoma huku ukijenga msingi wa Hisabati. Aidha, kitabu hiki kina sura kumi na sita zilizoandaliwa ili kukidhi mahitaji ya muhtasari wa soma la Hisabati Darasa la Tano.
Sura zilizoainishwa katika kitabu hiki ni pamoja na namba nzima, kujumlisha namba, kutoa namba, kuzidisha namba, kugawanya namba, namba za Kirumi, aina za namba, vigawo na vigawe, sehemu, desimali, vipeo na vipeuo, wakati, vipimo vya metriki, fedha ya Tanzania, jiometri, aljebra na takwimu.
Kwa kujifunza sura hizi, utaweza kujenga stadi zinazokuwezesha kutumia lugha ya Hisabati katika kuwasilisha hoja au wazo, kufikiri na kuhakiki katika maisha ya kila siku, na kutatua matatizo katika mazingira tofauti.
Hakikisha unafanya shughuli na mazoezi yote katika kitabu hiki ili uweze kupata umahiri uliokusudiwa. Shirikiana na wenzako katika kujifunza.
read less