Product description
Ni desturi ya utamaduni wetu wa kiafrika kusimulia, kutoka vizazi hadi vizazi, kumbukumbu za wazee wetu, familia zetu au watu wengine wa kihistoria waliotuachia urithi wa thamani na mafunzo. Usimulizi wa kile kinachokumbukwa ni njia muhimu ambapo his
..
read more
Ni desturi ya utamaduni wetu wa kiafrika kusimulia, kutoka vizazi hadi vizazi, kumbukumbu za wazee wetu, familia zetu au watu wengine wa kihistoria waliotuachia urithi wa thamani na mafunzo. Usimulizi wa kile kinachokumbukwa ni njia muhimu ambapo historia huweza kuhifadhiwa na kueleweka na wote. Kitabu hiki kinaangazia maisha ambayo yalikuwepo baina ya maeneo ya kijiografia yaliyokuwa na mawasiliano ya kipekee katika bahari ya Hindi. Kitabu kinaakisi zaidi maeneo ya Kilwa na Zanzibar kwa kupitia kumbukumbu za Salama binti Rubeya aliyekabili maisha kwa uvumilivu katika muktadha wa ustaarabu wa kilimwengu. Katika eneo ambalo historia simulizi ni sehemu ya maisha ya kila siku na hakuna mengi ambayo yameandikwa juu ya simulizi hizo, sauti ya Salama ni rejeo adimu la maisha kutoka miaka ya 1910 hadi 1960. Inaangazia mada mbalimbali zikiwemo za utambulisho na siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar. Kitabu hiki kina kumbukumbu za Salama binti Rubeya wa Kilwa na Zanzibar, aliyeolewa na Mohammed bin Abdulrahman Hamdani wa Mkunazini, Zanzibar, mama kwa Nafisa, Abdulrahman (Guy), Rabia, Abdulrahim, Mariam, Zakia na Salha (mwandishi mwenza wa kitabu hiki)
read less