Product description
Mwaka 2004 Profesa Wangari Maathai, kiongozi wa chama cha kuhifadhi mazingira (Green Belt Movement) nchini Kenya, alitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kupigana amani, demokrasia, utawala bora, matumizi
..
read more
Mwaka 2004 Profesa Wangari Maathai, kiongozi wa chama cha kuhifadhi mazingira (Green Belt Movement) nchini Kenya, alitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kupigana amani, demokrasia, utawala bora, matumizi sahihi ya mazingira na rasilimali kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijayo kote ulimwenguni. Zaidi ya mchango wake mkubwa katika utunzaji wa mazingira na kuhamasisha wanawake kutetea mazingira ambayo ndiyo msingi wa ustawi, Maathai, alijikuta katika migogoro kadhaa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii aliyopambana nayo katika kipindi chote cha maisha yake. Kutokana na matendo haya makuu, mwandishi Profesa Emmanuel Mbogo, ameona ni vyema kufungua dirisha la Historia, ili msomaji aweze kuchungulia na kupata dokezo kuhusu shujaa huyu ambaye dunia inamtambua ila yawezekana kuwa amesahaulika barani mwake.
read less