Tab Article
Kitabu hiki kinatoa mafunzo ya somo la Kiswahili kwa mujibu wa Muhtasari mpya wa Elimu ya Msingi kwa Darasa la 7 wa mwaka 2020. Uandaaji wa kitabu hiki umezingatia misingi na vigezo vya uandishi bora na umelenga kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuchambua mambo na kugundua maarifa mapya. Kitabu hiki kinatoa maarifa mbalimbali kuhusu ushairi, semi na msamiati. Vilevile, kuna maarifa kuhusu uandishi wa matini mbalimbali, kwa mfano insha, barua, risala na hotuba. Ndani ya kitabu hiki kuna vitendo na mazoezi mengi, ambavyo vinampa mwanafunzi fursa ya kujipima na kutendea kazi yale anayojifunza. Kupitia kitabu hiki, mwanafunzi ataweza kubobea katika umahiri mkuu wa aina tatu unaobainishwa na muhtasari, yaani kuwasiliana katika miktadha mbalimbali; kuonesha uelewa baada ya kusikiliza au kusoma; na kutumia msamiati katika miktadha mbalimbali.